© Goethe-Institut
Yiğit, Riesta, Simone, Eric na Imam wamekuwa wakiishi Ujerumani kwa muda fulani. Wanaelezea maisha yao katika makazi yao mapya. Kila mmoja wao ana hadithi tofauti.
Ujerumani , wanapitia mambo mengi ya kusisimua. Wakati mwingine wanapaswa kutatua hata matatizo madogo. Katika video unaweza kuona uzoefu wa vijana watano. Furahia.
Yiğit
Yiğit anatokea Uturuki. Anaishi Munich na anasoma huko. Yiğit anaishi katika bweni la wanafunzi. Pia ana mtu wa kubadilishana au kujifunza lugha. Mwenzake anataka kujifunza Kituruki na Yiğit anataka kuboresha Kijerumani chake.Kwa pamoja wanaweza kufanya mazoezi. Pia Yiğit huenda Stammtisch / meza au sehemu iliyoandaliwa kukutana na watu na kuzungumza Kijerumani.
Riesta
Huyo ni Riesta. Anatokea Indonesia. Sasa anaishi katika kijiji kidogo cha Berghausen. Anafanya kozi shirikishi( ya lugha na mwongozo) na anafanya kazi kama yaya katika familiya ya Kijerumani ambako anaishi. Katika muda wake wa ziada, huandika kwenye blogu kuhusu uzoefu wake Ujerumani.
Simone
Simone anatokea Brazil. Ameolewa na mtu wa Ujerumani na ana mtoto mdogo. Familia hiyo inaishi pamoja Möglingen. Hii ni sehemu ndogo. Simone anafanya kazi katika kampuni ya magari ya kijerumani. Humlea mtoto wake kwa lugha mbili. Baba huongea Kijerumani na mtoto na Simone huongea naye Kireno
Eric
Huyo ni Eric. Anatokea Kameruni na sasa anaishi Mannheim ambako anasoma pia. Eric anapenda kukaa na watu. Ndiyo maana , anaishi kwenye ghorofa pamoja na wengine. Hupenda kupika na wenzake anaoishi nao mapishi ya kimataifa na vyakula, haswa vya Ujerumani, kama vile Kohlrouladen/ kabichi iliyochemshwa yenye nyama .
Imam
Imam ametokea Indonesia. Na anaishi katika mji mkuu wa Ujermani, Berlin. Huko anasoma na kufanya kazi. Imam ni mkufunzi katika kituo cha utamaduni wa Indonesia. Anawasaidia watu wa Indonesia kujifunza Kijerumani na kuwasimulia historia kuhusu Ujerumani. Katika muda wake wa ziada , hutembelea vivutio vya Berlin.