Ein Kellner steht an der Bar in einem Restaurant und trocknet Gläser ab. © Goethe-Institut

Nyaraka muhimu kwa kuanza kazi

Umeshapata kazi ya kudumu? Basi wewe ni mwajiriwa. Unahitaji nyaraka kadha wa kadha kwa mwajiri wako. Kwanza unahitaji uthibitisho kuwa una bima ya afya. Unaweza kupata uthibitisho huu kutoka kwa kampuni ya bima.

Ujerumani kila mtu anatakiwa kuwa na bima ya kazi. Kwa kawaida unahitaji kadi ya taifa ya bima. Unaweza kupata hii pia kutoka kwa kampuni ya bima ya afya. Vile vile, Unahitaji mara kwa mara hati ya kibali cha polisi. Unaipata hii kutoka kwenye ofisi ya usajili wa wakazi.


Bima na kodi

Kama mwajiriwa una bima ya pensheni pia na bima ya kutokuwa na ajira. Lakini hautakiwi kufanya chochote kuhusu hilo, unazo hizi sera za bima. Mwajiri analipa sehemu ya bima hizi za afya, bima ya pensheni na bima ya kutoajiriwa. Unalipa iliyobakia. Inaponguzwa moja kwa moja kutoka katika ujira/mshahara wako. Unahitaji pia msimbo wa kodi na kadi ya kodi ya mapato ya kieletroniki. Unaweza kuzipa hizi zote kutoka ofisi ya kodi. Hautakiwi kufanya malipo ya kodi wewe mwenyewe. Ofisi za kodi zinachukua kodi kutoka kwenye ujira/mshahara wako.


Mkataba wa ajira

Kila mwajiriwa anapata mkataba wa ajira. Wewe na mwajiriwa mnasaini mkataba. Soma mkataba wa ajira, kuwa makini na maelezo. Na saini tu wakati ukiwa tayari. Kama hauna uhakika, uliza: watu wazima wanaweza kuuliza kwa Migrationsberatung für erwachsene Zuwanderer (Migration advice for adult immigrants; MBE). Watoto na vijana mpaka umri wa miaka 27 wanaweza kupata taarifa kutoka kwa Jugendmigrationsdiensten (youth migration services; JMD). Sheria zote zipo kwenye mkataba wa ajira. Wewe na mwajiriwa mnatakiwa kuzingatia sheria hizi. Taarifa nyingine zinatolewa hapa, kama vile: unapokea kiasi gani kila mwezi? Una mapumziko mangapi? Utafanya nini kama unaumwa?

Kwa kawaida, una muda wa kujaribu katika kazi mpya. Urefu wa muda wa kujaribu hutofautiana. Muda mwingine ni kwa wiki chache tu, muda mwingine miezi sita. Mwajiriwa anakuchunguza kwa karibu kwenye kipindi cha mda wa kijaribu. Anaamua kama utaendelea kufanya kazi katika kampuni baada ya muda wa kujaribu. Na unaamua kama unataka kuendelea na kazi hii baada ya muda wa kujaribu. Muda wa notisi ni ni mfupi wakati wa kipindi cha kujaribu (kwa kawaida wiki mbili au tatu), baada ya hapo ni kawaida miezi 3. 

Kazi ndogo

Ujerumani pia kuna kazi ndogo/kazi za Euro 520. Kazi ndogo ni kazi ambayo unaweza kupata mpaka Euro 520 kwa mwezi. Unapata moja kwa moja bima ya afya na bima ya pensheni ukiwa na na hizi. Lakini ni mwajiri pekee anayelipa michango hii, haulipi chochote. Hata hivuo, hauna bima ya kutofanya kazi.

Eine Kellnerin in einem Restaurant stellt Stühle auf die Tische. © Goethe-Institut


Ajira binafsi

Unafanya kazi kwa ajili yako, kwa maneno mengine wewe sio mwajiriwa? Basi unahitaji bima ya afya. Hata hivyo unatakiwa ulipie bima ya afya wewe mwenyewe. Pia, ni wazo zuri kuwa na bima ya pensheni. Katika baadhi ya kazi kama vile mafunzi na wakunga, ni lazima kuwa na bima ya pensheni. Nenda kwenye ofisi ya kodi na na omba namba ya kodi. Ofisi ya kodi watataka kujua makadirio ya faida yako ya mwaka. Basi inaweza kuamuliwa kiasi gani cha kodi ulipe. Unatakiwa kuhamisha pesa kutoka akaunti yako ya benki kulipa kodi. Kama unataka kuunda kampuni yako, unahitaji leseni ya biashara. Hii inapatika kutoka kwa ofisi ya leseni za biashara. Kwa mfano, hata kama unataka kufungua duka au mgahawa unahitaji leseni ya biashara.


Eine Frau sitzt an einem Tisch in ihrer Wohnung und arbeitet am Laptop. © Goethe-Institut

Video International Sign

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form