Ein junger Mann lehnt an einer Straßenlaterne und schaut auf sein Smartphone. © Goethe-Institut

Ushauri wa mtandaoni ni huduma inayotolewa na Jugendmigrationsdientse (Huduma ya uhamiaji kwa vijana; JDM)  Unaweza kuwasiliana na washauri kupitia mtandao na kuwauliza maswali yako . Timu ya washauri imekuwa ikifanya kazi kwa miaka mingi katika suala la kuwashauri wahamiaji. Wanatoa majibu kwa maswali yako yote kuhusu kuishi Ujerumani au matatizo unayoweza kukutana nayo pale. Kwa mfano, Ninaweza kupata wapi leseni ya udereva? Kazi kazi gani niayoweza kuifanya Ujerumani? Ninatakiwa kufanya nini?
Tovuti ya ushauri wa mtandaoni , www.jmd4you.de kwa sasa inapatikana kwa Kijerumani na Kituruki. Lakini lugha zifuatazo zitapatikana hivi karibuni: Kiingereza, Kiarabu, Kiserbia, Kialbania na Kirusi. Tayari inawezekana kuwauliza watu katika lugha hizi.

www.jmd4you.de

Namna ya kutumia mtandao huu;
Nenda online advice service website (huduma ya ushauri wa mtandaoni) na utaona picha hii:
Bonyeza kwenye moja ya vichwa vya habari katika hizo picha:
Utaona uwanda huu:
 

 
www.jmd4you.de Foto: © www.jmd4you.de

Bonyeza kitufe cha “Ingia”. Hapa unaweza kujisajili. Kisha bonyeza kitufe cha “Ombi jipya la awali”: 

 
www.jmd4you.de Foto: © www.jmd4you.de

Ingiza swali lako kwene uwanda huu. Mifano ya waswali imeoneshwa hapo chini ya uwanda. Hii itakusaidia wewe kutengeneza swali lako mwenyewe.

 
www.jmd4you.de Foto: © www.jmd4you.de

Ukishamaliza kutuma swali lako, utapokea jibu ndani ya masaa 24.Hautapata jibu hili kwenye akaunti yako ya kawaida ya barua pepe. Unatakiwa kurudi tena kwenye tovuti ya ushauri wa mtandaoni (online advise website). Kisha bonyeza  “mein JDM ( JDM yangi)”. Utapata majibu ya maswali yako pale.



Lakini unaweza tu kusima majibu ya maswali yako katika eneo la ushauri wa mtandaoni wa JDM. Ni salama na haioneshi jina. Hakuna atakayeona swali na jibu isipokuwa  wewe na mshauri.

Unaweza pia kuuliza maswali yako kwa njia ya kuchati au katika mijadala na huduma za ushauri wa mtandaoni za JDM. Japo hili huonesha jina. Unaweza  pia kuwasiliana na wahamiaji wengine kwa kuchati au katika mijadala ya mtandaoni. Kila mmoja anaweza kusoma maswali na majibu yako.

 

 
www.jmd4you.de Foto: © www.jmd4you.de

Sehemu ya “Maswali yanayoulizwa mara kwa mara-FAQ” ni mpya. Hapa yanapatikana majibu ya maswali ya kawaida. Unaweza pia kuuliza swali lako kuhusu mada za “Maswali yanayoulizwa mara kwa mara-FAQ”:

 
www.jmd4you.de Foto: © www.jmd4you.de

www.jmd4you.de