Ni shughuli zipi za burudani unazoweza kuzifanya? Vipo vingi sana vya kuchagua kuvifanya katika mji.
Utamaduni
Unapenda utamaduni? Katika miji mingi ya ujerumani na maeneo ya mijini kuna majumba ya makumbusho, sinema, kumbi na matukio mbalimbali ya tamasha. Sinema zinaongezeka sana kutazamwa katika matoleo asilia ya filamu za kimataifa. Unaweza kusoma vitabu, kusikiliza muziki, na kutazama filamu kwa malipo au pasipo kulipia. Unaweza pia kuazima vitabu, filamu na sidii, unakwenda nazo nyumbani kisha utayarudisha baadae.
Vituo vya elimu vya watu wazima, vyama na vilabu
Meneo mengi yana vituo vya elimu ya watu wazima, utakuta hasa kozi za watu wazima kwa mfano kozi za ngoma au kozi za lugha. Unaweza kutumia kiungo hichi kuweza kujua kituo cha elimu ya watu wazima kilichopo karibu na eneo unaloishi:
Kuna shughuli nyingi za bure kwa wazazi na watoto, kwa mfano baadhi ya miji ina viwanja vya kuchezea maalumu kwa watoto. Unapenda michezo? Vituo vya elimu ya watu wazima pia wanatoa kozi za michezo. Lakini waweza kwenda kwenye mabwawa ya umma ya kuogelea au kujiunga na vilabu vya michezo.
Chaguo lingine, ni kuweza kujiunga na vyama vyama vya michezo, vyama vinavyowaleta pamoja watu wenye malengo sawia na matakwa sawa. Kwa mfano kuna vyama vingi vya miziki, vyama vya michezo, vilabu vya ufumaji au vilabu vya kompyuta.
Vitu vya asili na mbuga za wanyama
Unafurahia kutoka nje kwa matembezi? Kuna mbuga kila mji. Kuna viwanja vingi vya watoto. Kwa kawaida unaweza kutembelea bure kabisa. Unaweza kuona mimea ya kawaida na gadeni za mimea, unaweza kutembelea pia wanyama wanaopatikana dunia nzima kwenye bustani za wanyama. Kwa kawaida kuna chagizo kwa ajili ya gadeni za mimea na bustani za wanyama. Mikoa mingi pie ina maziwa, misitu na milima na huenda hata unaishi karibu na bahari.
Nyumbani
Nyumbani watu wengi hufurahia kutazama filamu na kusikiliza redio. Kila nyumba ujerumani inatakiwa kusajili redio na televisheni yake na GEZ na kulipia kila mwisho wa mwezi. Kwa sasa inagharimu EURO 17.98 kwa mwezi. Kama huna pesa ya kutosha, haulazimiki kulipia chocote.
Pengine nyumba yako ina yadi au roshani, siku zote huruhusiwi kufanya kitu chochote maeneo hayo. Kwa mfano siku zote huruhusiwi kuwa na makutano yoyote kwenye roshani. Pitia kanuni za nyumba kwa taarifa Zaidi juu ya mambo haya.
Unaweza pia kupata taarifa juu ya nafasi za burudani za mitaani katika mji wako au tovuti ya jamii.
Video International Sign
maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.
Contact form