Man sieht eine Straße in Berlin mit vielen Menschen, die über die Straße gehen und einem Bus und Trams im Hintergrund. © Goethe-Institut

Kwa kutumia miguu na baiskeli 

Katika miji midogo na vijijini unaweza kufika mahali husika kwa kutembea kwa miguu. Katika nchi ya ujerumani watu wengi hutumia usafiri ili kuweza kufika mahali pa kazi na sehemu za kupata mahitaji muhimu. Barabara nyingi ni za lami. Mahali ambapo hakuna njia, watu hulazimika kutumia barabara za mitaa. Watoto wenye umri chini ya miaka 8 wanalazimika kutumia barabara. Na wale wenye umri chini ya miaka 10 wanashauriwa kutumia barabara. Kuna sheria za barabara zinazotumika kwa watembea kwa miguu na wanaotumia vyombo vya usafiri. Kwa mfano, ukiendesha chombo cha usafiri wakati taa nyekundu inawaka ama taa ya baiskeli yako ama taa ya chombo cha usafiri ikishindwa kufanya kazi na ukaonwa na polisi ni lazima ulipe faini.

Ansicht auf einen Gehweg mit abgestellten E-Rollern und Fahrrädern, im Hintergrund drei junge Männer und ein Schild einer Curry-Wurst-Bude. © Goethe-Institut

Usafiri wa umma 

Katika miji kuna usafiri wa umma kama vile treni za mikoa (S-bahn), reli za chini (U-bahn), trams (Straßenbahn, au Trambahn kusini mwa ujerumani) na basi. Kwa kawaida tiketi hununuliwa kwa kutumia mashine zilizopo stesheni na katika vituo vya kusafiria. Kuna ofisi maalumu za kununulia tiketi. Wakati mwingine unaweza kununa tiketi ndani ya gari. Pia unaweza kununua tiketi ya kutembelea kwa muda wa wiki, mwezi, au mwaka. Ni nafuu zaidi kutumia usafiri wa umma mara kwa mara. Watoto, wanafunzi,na abiria wenye ulemavu na wazee wao hulipa tiketi kwa kiwango cha chini cha pesa. Katika mabasi na treni huwa kuna ukaguzi wa tiketi. Ukigundulika kuwa hauna tiketi utatakiwa kulipa faini.

Katika stesheni na vituo vya mabasi huwa kunakuwa na ratiba. Ratiba huonyesha muda wakuondoka na kuwasili kwa mabasi na treni kituoni hapo. Lakini pia unaweza kupata taarifa kwenye tovuti ya kampuni ya chombo husika cha usafiri.

In einer Unterführung sieht man ein Fahrrad, zwei E-Roller und beklebte Säulen, im Hintergrund fährt eine Tram vorbei. © Goethe-Institut

Usafiri binafsi     

Watu wengi mijini pia wanatembea kwa kutumia usafiri binafsi. Miji mingi ina vituo vya magari binafsi na magari na multi storey: hizi ni ishara pembeni mwa bara bara kuonyesha mahali vituo vya maegesho ya magari. Unapoendesha gari, ni muhimu kuwa na leseni na hati ya usajili. Ikiwa umesimamishwa na polisi atahitaji kuona taarifa hizo.

Kutembelea maeneo mengine zaidi 

Je unahitaji kutembelea miji ya ujerumani na nje ya ujerumani? Unaweza kutumia treni, ndege au basi. Kituo cha mabasi kipo karibu na stesheni ya reli mara nyingi ni mijini/ kwenye majiji.

Kwa safari ndefu, kuna mabasi ya umbali mrefu. Kuna watoa huduma mbalimbali Ujerumani. Wanasafiri katika miji kadha wa kadha Ujerumani na Ulaya. Kama ukikata tiketi mapema, tiketi inaweza kuwa ya bei nafuu. Mabasi ya umbali mrefu ni ya starehe sana na mara nyingi unapata Wi-Fi.  Basi lipi linaenda lini na wapi, unaweza kufahamu kupitia www.fernbusse.de.
 
Kwa kawaida Deutsche Bahn (DB) kwa safari ndefu hutumia usafiri wa treni. Kwa kawaida kunakuwa na punguzo. Kama utakata tiketi mapema unaweza kupata kwa bei nafuu. Hii ni sawa na usafiri wa anga. Meli kubwa pia huondoka kwenda visiwa vilivyopo bahari ya kusini mwa baltiki.

Ansicht auf ein Bahnhofsgebäude, oben ist ein abgeschnittenes Deutsche Bahn-Logo zu sehen, außerdem Wegweiser zu den Gleisen. © Goethe-Institut

Video International Sign

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form