Kuanzia kuzaliwa hadi miaka 3
Wewe na mwenza wako mnafanyakazi na mna mtoto (mwenye miezi hadi umri wa miaka 3)? Halafu unampeleka mtoto wako sehemu za kuangalia watoto. Sehemu zenyewe ni chache. Kutokana na sababu hiyo unashauriwa kumwakikisha mapema iwezekanavyo. Kuanzia umri wa miaka 3 mtoto anaweza kuanza shule ya awali. Huko wanacheza, wanaimba, kupaka rangi na kufanya shughuli nyingi za mikono. Shule nyingi za awali. Katika shule nyingi za awali walezi wa watoto huwapeleka watoto michezoni katika kipindi cha kiangazi. Shule za awali mara nyingi hufundisha lugha kwa ajili ya kuwasaidia watoto. Kwa mfano, watoto hucheza michezo inayohusiana na lugha na pia husoma hadithi.
Shule za awali na vituo vya kulelea watoto
Shule za awali huwaandaa watoto kwa ajili ya kuanza shule rasmi. Kila mtoto mwenye umri wa miaka 3+ ana haki ya kupelekwa shule. hata katika jamii ndogo pia kuna elimu za awali. Mwandikishe mtoto wako katika muda wa kutosha. Kupitia elimu ya awali mtoto pia hujifunza mambo yanayohusu tamaduni na ataweza kufahamu kwa haraka kuhusu nchi.
Baadhi ya shule za awali huanza vipindi (saa 1:00 asubuhi hadi saa 6:00 au saa 7:00 mchana). Nyingine huanza vipindi (saa1:00 asubuhi hadi saa 10:00 au 11:00 jioni). Shule hizi hujulikana kama kita (Kindertagesstätte; vituo vya kulelea watoto). Mtoto wako atapata lunch hapo hapo. Kwa kawaida unatakiwa kulipia eneo ambalo mtoto wako analelewa, au sehemu ya elimu ya awali/vituo vya kulelea watoto.
Gharama zinatofautiana kutokana na hali ya mtu na mwingine. Na si wote wanalipa gharama sawa. Hii inategemeana na sababu mbalimbali: kiasi gani cha pesa unacholipwa? Mtoto wako ana umri gani? Na pia masaa mangapi shuleni? Kuna vituo vinavyoendeshwa na serikali na vituo vya watu binafsi. Vituo vya kulelea watoto vya binafsi vina gharama kubwa sana. Baadhi ya vituo vya binafsi huzungumza lugha mbili mfano: kispanishi na kijerumani.
Katika vituo vingi kuna lugha ambayo kila mtoto anatakiwa aijue kabla ya kuanza shule rasmi. Wakati mwingine kijeruma ni kigumu hata kwa watoto wa kijerumani. Mwanafunzi atakayeshindwa jaribio atapaswa kurudia mwaka mwingine au kupewa msaada wa kujifunza lugha .
Video International Sign
Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.
Contact form