Kibali cha kufanya kazi
Je umetokea nje ya Umoja wa Ulaya (EU) au ukanda wa kiuchumi wa Ulaya ? Hivyo, unahitaji kibali cha kufanya kazi Ujerumani. Mataifa ya nchi za EU Romania na Bulgaria wanahitaji kibali cha kufanya kazi mpaka mwisho wa mwaka 2018, lakini sio baada ya muda huo.
Endapo umeruhusiwa kufanya kazi Ujerumani na kwa muda gani, inaonyeshwa kwenye kibali chako cha makazi.
Vyeti na Utambuzi
Je una sifa za kiufundi, shahada ya Chuo Kikuu au cheti cha shule kutoka katika nchi yako? Unatakiwa kuwa na hivi vyeti/nyaraka ambazo zimetafsiriwa na kuthibitishwa.Uthibitisho unamaanisha kuwa mamlaka rasmi imehakiki nyaraka zako na kuona kuwa ni za kweli. Mahali pazuri pakufanikishiwa jambo hili ni katika malamka iliyopo katika nchi yako. Muda mwingine sifa zako zinaweza kuwa si halali Ujerumani. Unaweza kuangalia hili jambo wakati ukiwa nchini mwako (Utambuzi wa sifa za kigeni). Unaweza kupata taarifa zaidi kupitia tovuti ya
. Pia ,tazama infografiki zetu hapa.Nafasi za kazi
Umeshapata kibali cha kufanya kazi? Hivyo, unaweza kutafuta kazi.Kuna mianya mingi sana: unaweza kutafuta kazi zinazotangazwa mitandaoni, kwenye magazeti au kwa wakala wa ajira/kitengo cha ajira. Kwa kawaida, utaona kazi za kawaida kwenye magazeti. Lakini matangazo yanaenda kwa wakati. Kuna kazi nyingi zinazotangazwa kwenye mitandao, lakini mara nyingi haziendi kiwakati. Kitengo cha ajira kitakushauri na kukutafutia kazi stahili kwa ajili yako. Lakini unaweza kwenda moja kwa moja kwenye makampuni. Muda mwingine wanakuwa na nafasi za ajira, lakini hazipo kwenye mtandao au kwenye magazeti. Muda mwingine unaweza kutafuta nafasi za ajira kwenye tovuti ya kampuni.
Pia, kuna BIZ (Kitengo cha ushauri wa kazi) katika wakala wa ajira: utaangalia matangazo ya ajira hapo pamoja na taarifa kedekede juu ya dhana za ajira na kazi.Unaweza kutuma maelezo yako mafupi hapo kwenye mtandao, hata pia katika kitengo cha ajira. Kitengo cha BIZ kinatoa huduma za ushauri wa ajira kama endapo haufahamu nini unachoweza au kutaka kufanya.
Mtawanyo wa kazi katika kampuni ni mzuri: unapata kujua kazi na unaweka mawasiliano.
Maombi
Maombi yako ni hatua ya kwanza katika soko la ajira. Nyaraka za maombi ni za umuhimu sana. Unatakiwa uwe na barua ya ushawishi (barau kwa kampuni), picha nzuri ya maombi, wasifu binafsi na vyeti vyako (katika kijerumani). Kitengo cha BIZ kinatoa warsha za “kuomba kazi Ujerumani’’. Unajifunza namna maombi ya kazi yanavyokuwa na namna gani ya kujiandaa kwa ajili ya mahojiano ya ajira.
Miji mingi ina huduma za ushari kwa wahamiaji. Hapa, watakusaidia kutafuta ajira na kuandika maombi ya kazi (tazama Bundesamt für Migration Bundesamt für Migration und Flüchtlinge). Ushauri maalum unapatika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 27 kutoka kwa huduma za uhamiaji kwa vijana.
Tovuti husianishi
Video International Sign
Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.
Contact form