Hati ya kusafiria na Viza
Kwa ajili ya kusafiri kwenda Ujerumani, unahitaji hati ya kusafiria halali na nyaraka nyingine halali ambazo zinathibitisha utambulisho wako.Utahitaji hati ya kusafiria baadae pindi utakapoenda kudahiliwa katika mamlaka.Wakazi wa nchi nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wanahitaji pia viza.
Unaweza kuomba viza katika ubalozi wa Ujerumani nchini mwako. Je, umeshapata tayari mkataba wa ajira UJerumani, au una wanafamilia wanaoishi hapo? Basi, itakuwa rahisi kupata viza. Unaweza kupata taarifa kutoka Federal Foreign Office.
Wananchi kutoka EU au nchi yoyote iliyopo katika Ukanda wa Kiuchumi wa Ulaya hawaitaji viza.
Ofisi ya Udahili wa Wakazi na Kibali cha makazi
Ukiwa Ujerumani unatakiwa ujisajili katika Einwohnermeldeamt (Ofisi ya udahili wa wakazi) katika mji au jiji lako la makazi. Baadae, unatakiwa uende kwa Ausländeramt (Ofisi ya uhamiaji). Hapo utapatiwa hati ya makazi. Ni kadi inaonyesha hadhi yako ya makazi. Inaonyesha muda gani unaruhusiwa kubaki Ujerumani na kama unaruhusiwa kufanya kazi.
Je, unahitaji kutembelea ofisi, lakini huwezi kuzungumza kijerumani vizuri? Basi, unaweza kumwomba mkalimani. Ni yule ambaye anaweza kuongea kijerumani na lugha yako na atakusadia kuwasiliana.
Kozi shirikishi
Kama hauwezi kuongea kijerumani vizuri sana, basi unaruhusiwa kufanya kozi shirikishi. Muda mwingine, unatakiwa kufanya kozi shirikishi. Utajifunza kijerumani kizuri katika kozi. Na utapatiwa taarifa muhimu kuhusu maisha ya Ujerumani. Ofisi ya Uhamiaji itakupatia kwa ajili ya kozi na itakwambia wapi utaweza kufanya kozi. Unaweza kuisoma zaidi kwa kufuata kiungo cha kozi shirikishi.
Kutafuta ajira na mafunzo ya kiufundi
Hatua ifuatayo ni kutafuta kazi. Ulishasoma tayari taaluma hiyo nchini mwako, au ulishawahi kuwa chuo kikuu? Basi, unatakiwa kuwa na nyaraka zilizotafsiriwa na kuthibitishwa.Uliza wapi unaweza kuifanya katika wakala wa ajira. Wakala wa ajira watakusaidia kutafuta ajira.Kama bado hauna taaluma au sifa za kuondoka shule, unatakiwa uende pia kwa wakala wa ajira. Watakupatia ushauri wa kazi. Watakusaidia kama hauna uhakika juu ya aina ya kazi ungependelea kufanya au ungeweza kuifanya.Wakala wa ajira watakupatia taarifa kuhusu mafunzo na kozi. Unaweza kupata taarifa zaidi katika ukurasa wa Utafiti wa kitaalumana mafunzo ya ufundi.
Watoto na Shule
Watoto kuhudhuria shule. Msajili mtoto wako katika shule. Jugendamt (ofisi ya vijana) katika mji/jiji lako inaweza kukusaidia. Soma zaidi katika kurasa zifuatazo: elimu ya wali na mfumo wa shule.
Bima
Baadhi ya mipango ya bima ni muhimu sana hasa bima ya afya, bima ya pensheni na bima ya huduma (tazama ukurasa wa bima). Kama una kazi, utahakikishiwa moja kwa moja mipango hii (tazama ukurasa wa kuanza kazi). Na unahitaji akaunti ya sasa katika benki (tazama akaunti ya benki na fedha).
Video International Sign
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.
Contact form