Unataka ...
- kujiandaa kusoma nchini Ujerumani,
- kuonyesha ufahamu wa hali ya juu wa lugha ya Kijerumani kwa ajili ya kazi,
- kujiandaa kufanya kazi katika sekta ya afya nchini Ujerumani,
- kuthibitisha mafanikio yako ya kujifunza katika daraja C1,
- kupata cheti kutoka Taasisi inayotambulika kimataifa?
Goethe-Zertifikat C1 ni mtihani wa Kijerumani kwa watu wazima. Unathibitisha kuwa watahiniwa wamepata ustadi zaidi wa kuongea lugha ya Kijerumani na unakidhi vigezo vya hatua ya tano (C1) katika ngazi ya hatua sita za uhadari zilizowekwa na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
Kufaulu mtihani inamaanisha kuwa unaweza …
- kuelewa kwa mapana maneno magumu na marefu ikiwa ni pamoja na maana zinazojitokeza bila kutajwa
- kujieleza kwa ufasaha na usahihi bila kusitasita wala kuhitaji kusaka maneno,
- kutumia lugha kikamilifu na kwa kunyumbulika kazini au katika jamii au wakati wa mafunzo au masomo yako
- kutoa kauli zinazoeleweka wazi, zilizonyooka na zenye maelezo ya kina unapoongelea mada nzito
Tafadhali wasiliana na chuo kikuu, taasisi ya elimu ya juu au mtoaji wa kozi ya maandalizi kabla ya kuanza kwa kozi yako ili kubaini endapo mtihani wa Goethe-Zertifikat C1 utakidhi vigezo vya kukusamehe kufanya mtihani wa lugha kwa ajili ya kujiunga na chuo kwa wanafunzi wa kigeni.
matini ya mazoezi
Hapa utapata aina na seti za mazoezi kwa ajili ya kufanya majaribio mtandaoni, pia bila vizuizi na kwa mwingiliano.
Maelezo zaidi
Vigezo, maudhui ya mtihani na maelezo zaidi kuhusu mtihani wa Goethe-Zertifikat C1 yanaweza kupatikana hapa: