Goethe-Zertifikat A2

Unafaa endapo unataka

  • kuonesha kuwa una kiwango cha msingi cha uelewa wa Kijerumani 
  • kuthibitisha kuwa umefaulu kufika hatua A2
  • kupata cheti rasmi kinachotambulika kimataifa

Goethe-Zertifikat A2 ni mtihani wa Kijerumani kwa watu wazima. Unahitaji uelewa wa awali wa stadi za lugha na unakidhi vigezo vya hatua ya pili (A2) katika ngazi ya hatua sita za uhadari zilizowekwa na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).

Kufaulu mtihani inamaanisha kuwa unaweza …

  • kuelewa na kutumia sentensi na maneno ya kawaida ya kila siku,
  • kueleweka unapoongea katika mazingira yanayohitaji kutoa na kupokea taarifa nyepesi juu ya mambo yaliyozoeleka
  • kuelezea historia yako na elimu yako, mazingira yaliyokuzunguka kwa karibu na mambo mengine yanayohusu mahitaji yako, kwa njia rahisi

Maandalizi

Matini ya mazoezi

Mitihani ya mfano na matini ya kufanyia majaribio ambazo ni rahisi kutumia kukusaidia mtandaoni vinapatikana hapa

Maelezo zaidi

Mahitaji, yaliyomo katika mtihani na maelezo zaidi juu ya mtihani wa Goethe-Zertifikat A2 yanapatikana hapa: