Unafaa endapo unataka
- kujiandaa kusoma kwenye chuo kikuu au taasisi ya elimu ya juu nchini Ujerumani
- kutoa ushahidi wa ustadi zaidi wa Kijerumani kwa ajili ya maombi ya kazi
- kujiandaa kufanya kazi katika fani ya afya nchini Ujerumani
- kutoa ushahidi kuwa umefaulu hatua ya B2
- kupata cheti rasmi kinachotambulika kimataifa
Goethe-Zertifikat B2 ni mtihani wa Kijerumani kwa vijana na watu wazima. Unathibitisha kuwa watahiniwa wamepata ustadi zaidi wa kuongea lugha ya Kijerumani na unakidhi vigezo vya hatua ya nne (B2) katika ngazi ya hatua sita za uhadari zilizowekwa na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
Kufaulu mtihani inamaanisha kuwa unaweza …
- kuelewa mambo makuu kutoka kwenye maandishi yaliyo katika lugha au mada ngumu, na pia majadiliano ya kiufundi katika eneo la utaalamu wako,
- kuwasiliana kwa kuongea bila kusita kiasi kwamba mazungumzo ya kawaida na mzungumzaji wa asili ya Kijerumani yanawezekana bila ya kuhitaji juhudi kubwa kutoka upande wowote,
- kutoa maoni yako juu ya masuala yanayoendelea katika jamii katika lugha inayoeleweka na maelezo ya kina, kuelezea msimamo wako juu ya mambo hayo na na kutaja faida na hasara kutoka maoni mbalimbali
Matini ya mazoezi
Mitihani ya mfano na matini ya kufanyia majaribio ambazo ni rahisi kutumia kukusaidia mtandaoni vinapatikana hapa
Maelezo zaidi
Mahitaji, yaliyomo katika mtihani na maelezo zaidi juu ya mtihani wa Goethe-Zertifikat B2 yanapatikana hapa: