Kusoma Ujerumani

Huduma ya ushauri (chuo kikuu) © Picha: Goethe-Institut/Bernhard Ludewig  Huduma ya ushauri (chuo kikuu) Picha: Goethe-Institut/Bernhard Ludewig
Je wajua kwamba miaka mia moja iliyopita 50% ya watu waliosoma ng'ambo walikuwa wanasoma nchini Ujerumani? Ujerumani imewavutia watu waliotafuta elimu ya hadhi ya juu tokea zama hizo.

Kuna sababu nzuri ya Kusoma Ujerumani:
  • Chuo kikuu cha kwanza nchini Ujerumani kilifunguliwa Heidelberg mwaka 1386. Leo unaweza kuchagua kati ya taasisi zaidi ya 300  za elimu ya juu zinazotoa elimu ya hadhi ya juu.
  • Ikiwa na takribani waongeaji wa asili million 100, Kijerumani ni lugha inayozungumzwa zaidi barani Ulaya. Nguvu za kiuchumi za Ujerumani na ushawishi wake unaoongezeka dunia vinafanya Kijerumani lugha inayoendelea kuwa muhimu zaidi kwenye soko la dunia.
  • Gharama za maisha kwa wanafunzi huweza kushuka kutokana na wigo wa msaada.
  • Pamoja na wigo mpana wa shughuli za kujipumzisha kwenye vyuo vikuu kuna fursa nyingi nje ya vyuo za kufurahia michezo, utamaduni au shughuli nyingine kadha wa kadha.

Kozi za masomo kimataifa

Vyuo vikuu vingi vya Kijerumani hutoa kozi zinazoongoza kimataifa kutambuliwa kwa sifa, na hutoa wigo mpana wa uchaguzi: astashahada, shahada, shahada za uzamivu na shahada za uzamili. Kozi zote huzingatia viwango vya juu vya taaluma na zimepangiliwa vizuri; zinafundishwa kwa Kiingereza na nyongeza ya kozi za Kijerumani.
Juu