The
www.pasch-net.de tovuti imegawika katika sehemu tatu:
- Eneo kuu
- Eneo la walimu
- Eneo la Wanafunzi
Eneo kuu
Eneo kuu natoa taarifa kuhusu taasisi washirika na shughuli zao. Shughuli hizi zinajumuisha miradi midogo ilimo katika utaratibu wa mradi wa PASCH, blogu za wafanyakazi kutoka ofisi mbalimbali za kikanda duniani, kozi za PASCH kwa vijana nchini Ujerumani na jukwaa ambalo mashule huweza kupata shule za kuanzisha undugu kutoka nchi mbalimbali. Ramani ya kuvutia ya ulimwengu inaonesha mtandao wa shule washirika, na shule washirika huweka kwa kifupi taarifa zinazotoa picha juu yao.
Eneo la walimu
Katika eneo hili, walimu huweza kupata dhana au fikra juu ya kutumia PASCH-net katika vipindi vyao vya somo la Kijerumani, kupakua matini ya kufundishia na kupata taarifa kuhusu mbinu na maarifa ya ufundishaji. Jukwaa la mafunzo la PASCH huwawezesha walimu kufanya maandalio kwa njia ya mtandao au kutumia kozi zilizopo.
Kama jamii, walimu huweza kushirikisha matini yao au kupata washirika kwa ajili ya kutimiza fikra juu miradi yao. Kupitia jumuiya, jukwaa la mafunzo na blogu, walimu huweza kutekeleza miradi ya kimataifa kama vile magazeti kwa njia ya mtandao pamoja na vipindi vya sauti.
Kwenye jukwaa la mafunzo la PASCH, PASCH-net hutoa kozi za ziada ya mafunzo zinazofundishwa kwa njia ya mtandaokwa walimu. Kupitia kozi ya mtandaoni ya PASCH-net-Führerschein, walimu hujifunza kuhusu manufaa ya tovuti hiyo katika vipindi vyao vya lugha ya Kijerumani, kama vile jumuiya, jukwaa la mafunzo na gazeti la kimataifa la PASCH kwa mashule. Kupitia kozi ya mtandaoni ya Moodle-Führerschein wanajifunza jinsi jukwaa la mafunzo la PASCH, linalotumia programu za Moodle, linavyoweza kutumika katika vipindi vya shule au wakati wa kozi za mafunzo ya ualimu.
Mawasiliano:
lernplattform@pasch-net.de
Eneo la wanafunzi
Wanafunzi wanaosoma lugha ya Kijerumani kwenye shule za PASCH huweza kushirikishana mawazo na mitazamo yao na wanafunzi kutoka jumuiya nyingine. wanaweza pia kutuma machapisho, picha na video, kujiunga katika vikundi na kutengeneza jukwaa la majadiliano.
Mashindano na miradi huwapa moyo vijana kushiriki. Machapisho katika hatua tofauti za ugumu wa lugha hutoa taarifa kuhusu Ujerumani, ikiwemo uwezekano wa kwenda huko masomoni.
Mada za majadiliano, shughuli na michezo ya lugha kwa wanafunzi wa Kijerumani.
Yeyote anayetaka kuchangia kwenye jumuiya au jukwaa la kujifunza la PASCH-net anapaswa kujisajili na kuingia kwa kutumia anuani ya baruapepe na nenosiri.
Mawasiliano:
service@pasch-net.de