Goethe-Zertifikat C1
Goethe-Zertifikat C1 ni mtihani wa Kijerumani kwa watu wazima. Unathibitisha kuwa watahiniwa wamepata ustadi zaidi wa kuongea lugha ya Kijerumani na unakidhi vigezo vya hatua ya tano (C1) katika ngazi ya hatua sita za uhadari zilizowekwa na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
Kufaulu mtihani inamaanisha kuwa unaweza …
- kuelewa kwa mapana maneno magumu na marefu ikiwa ni pamoja na maana zinazojitokeza bila kutajwa
- kujieleza kwa ufasaha na usahihi bila kusitasita wala kuhitaji kusaka maneno,
- kutumia lugha kikamilifu na kwa kunyumbulika kazini au katika jamii au wakati wa mafunzo au masomo yako
- kutoa kauli zinazoeleweka wazi, zilizonyooka na zenye maelezo ya kina unapoongelea mada nzito