Goethe-Zertifikat A2
Goethe-Zertifikat A2 ni mtihani wa Kijerumani kwa watu wazima. Unahitaji uelewa wa awali wa stadi za lugha na unakidhi vigezo vya hatua ya pili (A2) katika ngazi ya hatua sita za uhadari zilizowekwa na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
Kufaulu mtihani inamaanisha kuwa unaweza …
- kuelewa na kutumia sentensi na maneno ya kawaida ya kila siku,
- kueleweka unapoongea katika mazingira yanayohitaji kutoa na kupokea taarifa nyepesi juu ya mambo yaliyozoeleka
- kuelezea historia yako na elimu yako, mazingira yaliyokuzunguka kwa karibu na mambo mengine yanayohusu mahitaji yako, kwa njia rahisi