Goethe-Zertifikat B1
Goethe-Zertifikat B1 ni mtihani wa Kijerumani kwa vijana na watu wazima. Unathibitisha kuwa watahiniwa wamepata ustadi wa kuongea lugha ya Kijerumani na unakidhi vigezo vya hatua ya tatu (B1) katika ngazi ya hatua sita za uhadari zilizowekwa na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
Kufaulu mtihani inamaanisha kuwa unaweza …
- kuelewa vidokezo muhimu vya taarifa katika maongezi na maandishi juu ya mambo yaliyozoeleka yanayohusiana na kazi, shule na muda wa burudani, nk. Pale yanapofanyika kwa kutumia lugha sanifu,
- kujihudumia mwenyewe katika hali mbalimbali unaposafiri kwenye nchi zinazoongea Kijerumani,
- kujielezea mwenyewe kwa njia rahisi unapoongelea mambo yaliyozoeleka na mambo unayoyapenda,
- kutoa taarifa ya uzoefu fulani au matukio, kuelezea ndoto zako, matarajio na matamanio pamoja na sentensi fupi za ufafanuzi.