- Ada yote ya kozi italipwa wakati wa kujiandikisha kozi kwa kuiweka kwenye akaunti yetu ya Benki (tazama taarifa ya akaunti chini).
- Risiti lazima iwasilishwe kwa mwalimu wadarasa au ofisi ya usajili siku ya kwanza ya darasa.
- Idadi ya juu ya wanafunzi kwa kila darasa ni 20 na ya chini ni 12. Madarasa yanaweza kuahirishwa, au madarasa ya daraja moja kuunganishwa katika kipindi cha muhula. Iwapo darasa litaahirishwa na Goethe-Institut na kukawa hakuna darasa lingine la daraja hilo, ada ya kozi ya wanafunzi husika itatumika kwenye muhula unaofuata. Ikiwa usajili hautafikia idadi ya chini ya wanafunzi hadi kufikia tarehe ya kuanza kozi, Goethe-Institut inabaki na haki ya kubadili aina ya kozi, muundo au tarehe ya kuanza kwa kushauriana na washiriki wa kozi.
- Kutakuwa na makato ya 20% ya ada ya iliyolipwa iwapo utaghairi kufanya kozi siku saba kabla ya kozi kuanza. Pesa haitarudishwa punde tu kozi itakapoanza. Taarifa ya kutofanya kozi lazima iwasilishwe Goethe-Institut Tanzania kwa Barua pepe au iletwe na Mtu kwa maandishi. Tarehe ya kughairi kufanya kozi itakuwa ni tarehe ya kupokea katika Goethe-Institut Tanzania.
- Wanafunzi lazima wawe wametimiza umri wa miaka 16 wakati wa kujiandikisha.
- Usajili kwenye wavuti yetu mtandaoni "Mein Goethe.de" ni lazima kwa wanafunzi wote.
- Wanafunzi wote wa kigeni lazima waombe kibali cha kuishi cha mwanafunzi kutoka Idara ya Uhamiaji.
- Usajili hauwezi kuhamishwa kutoka mtu mmoja Kwenda kwa mwingine. Mabadiliko ya darasa yanahitaji idhini ya Mkuu wa Idara ya Lugha.
- Kuandikishwa kwa ngazi inayofuata kunategemea kufaulu kwa majaribio ya tathmini endelevu au mitihani ya mwisho wa kozi. Alama za kufaulu kwa mitihani na mitihani yetu ni 60%. Cheti cha B1 kinahitajika ili kuingia kwenye darasa la B2.1.
- Vyeti vya uthibitsho wa kuhudhuria vitatolewa mwishoni mwa kozi ikiwa tu mahudhurio ya mwanafunzi yamefikia 80% au zaidi.
- Vyeti vilivyopotea haviwezi kutolewa upya. Barua ya uthibitisho itatolewa katika tukio la cheti kilichopotea baada ya kuonesah taarifa ya upotevu toka polisi.
- Ukaguzi wa usalama ni wa lazima kwa wanafunzi na wageni wote wanapoingia kwenye lango kuu la Goethe-Institut tanzania.
- Wanafunzi wanashauriwa kukata bima ambayo itawahudumia katika matukio ya dharura. Wale walio na matatizo ya kudumu ya kiafya wanapaswa kuwafahamisha walimu wao ili Goethe-Institut iweze kuita usaidizi wa dharura ikihitajika. Gharama zozote zinazotokana na dharura za matibabu zitagharamiwa na mwanafunzi au wazazi/walezi wao.
- Washiriki wote wa Kozi na Mitihani watasaini vigezo na masharti ya utunzaji wa taarifa binafsi ili kutoa idhini ya uwasilishaji wa taarifa hizo binafsi kwenye makao makuu ya Goethe-Institut huko Munich, Ujerumani.
- Washiriki wa kozi na Mithani wanaofadhiliwa watasaini makubaliano ya kuwapatia wafadhili wao taarifa ya maendeleo ya kozi ikiwa ni pamoja na mahudhurio au matokeo yao ya mitihani.
- Dhima ya Taasisi ya Goethe na wafanyakazi wake itakubalika tu iwapo kuna uzembe au makusudi na kutojali. Goethe-Institute haitakubali dhima yoyote ya kusitisha au kuahirisha huduma zake kunakotokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake au kunakosababishwa na hali zingine zote zilizo nje ya udhibiti wake.
Taarifa za Akaunti:
Jina la Akaunt: GOETHE-INSTITUT
Account in Tanzania:
National Bank of Commerce (NBC),
Dar es Salaam
Account No. 012103020424
SWIFT NLCBTZTXXXXX
Course fees, Name/Surname
Account in Germany:
Commerzbank München
IBAN
DE17 7004 0041 0227 5972 00
SWIFT-BIC COBADEFFXXX
Betreff: Kursgebühren, Name
Copyright @ Goethe- Institut
Alle Rechte vorbehalten
www.goethe.de/tanzania