Goethe-Zertifikat C2: GDS
Goethe-Zertifikat C2: Großes Deutsches Sprachdiplom ni mtihani wa Kijerumani kwa watu wazima. Unathibitisha kuwa watahiniwa wamepata ustadi mkubwa sana wa kuongea lugha ya Kijerumani na unakidhi vigezo vya hatua ya sita (C2) katika ngazi ya hatua sita za uhadari zilizowekwa na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
Kufaulu mtihani inamaanisha kuwa unaweza …
- kuelewa bila taabu yoyote karibu kila kitu unachosoma au kusikia katika Kijerumani,
- kufanya muhtasari wa maelezo yaliyoandikwa au kusemwa, ukizingatia mantiki ya sababu na maelezo hayo
- kujieleza kwa kwa kiwango cha juu cha ufasaha na usahihi na kutoa ufafanuzi mzuri wenye kuleta maana wakati wa kujadili mada nzito
Mtihani unatambulika kama ushahidi rasmi wa uhodari wa lugha unaohitajika kufundisha Ujerumani kote. Maelezo ya ziada kuhusu suala hili yanapatikana kutoka taasisi zinazotambuliwa katika kila jimbo nchini Ujerumani, kama vile Wizara ya Elimu na Utamaduni, Ofisi ya Mafunzo ya Ualimu, Halmashauri ya Wilaya au Kamati ya Seneti
Kuanzia tarehe 1 Januari 2012, mtihani wa Goethe-Zertifikat C2: Großes Deutsches Sprachdiplom ulianza kutumika badala ya mitihani mitatu iliyokuwa ikitumika kabla, ambayo ni Goethe-Zertifikat: Zentrale Oberstufenprüfung (ZOP), Kleines Deutsches Sprachdiplom (KDS) na Großes Deutsches Sprachdiplom (GDS).