Ujauzito
Maisha ya mtoto huanza wakati wa ujauzito. Ili kufahamu vizuri suala la ujauzito. Ni vizuri kwenda kuonana na watoa huduma na washauri wa suala hilo. Inashauriwa kuonana na mtaalamu mara kwa mara kipindi cha ujauzito. Yeye anaweza kujibu maswali na kukuelekeza jinsi ya kutunza afya ya mtoto. Mkunga pia ana wajibu sawa na daktari. Anaweza kukusaidia kipindi chote cha ujauzito hadi kujifungua. Daktari wako pia anaweza kukusaidia kutafuta mtaalamu na/au mkunga. Wanawake wengi pia wanashauriwa kuhudhuria kliniki baada ya kujifungua. Huko utapata maelekezo ya jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya uzazi. Na pia kuweza kufahamu wanawake wengine ambao ni wajawazito.
Sheria zinazowalinda wafanyakazi wa kike, likizo ya uzazi na malipo yake
Kwa mwenye kazi ya kudumu, anapata faida ya Mutterschutz (sheria zinazowalinda wafanyakazi wa kike) hata kabla ya uzazi kwa maneno mengine wanakuwa mapumzikoni. Mara nyingi huchukua wiki sita (6) ina maana kabla ya uzazi. Likizo ya uzazi chini ya sheria ya Mutterschutz huishia kwa kipindi cha wiki 14. Kipindi hiki kinaweza kikaongezeka pia mwajiri wako hawezi kuvunja mkataba wakati wa kipindi hiki. Baada ya likizo ya Mutterschutz. Baada ya likizo ya uzazi unaweza kuongeza muda hadi mtoto atakapofikisha umri wa miaka mitatu (3). Baada ya miaka mitatu hiyo unaweza kurejea tena kazini.
Katika kipindi cha miezi 12 ya kwanza ya uzazi unalipwa malipo ya uzazi. Na kama mwenzako atachukua likizo ya uzazi, itaongezeka hadi miezi 14. Malipo hayo ya uzazi yanategemeana na kiwango chako cha mshahara kwa mwezi. Unatakiwa kuomba malipo hayo au posho hiyo. Pia malipo hayo yanaweza kulipwa hata kama sio mwajiriwa. Zaidi ya malipo hayo, pia unaweza kuomba gharama za malezi ya mtoto. Utapata gharama hizo hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka nane. Kwa ambao hupata pesa kidogo, huweza kupata kwa masharti fulani, pesa ya ziada kwa manufaa ya mtoto.
Huduma za afya
Ni vizuri kuonana na daktari wa watoto mara kwa mara. Daktari atanukuu kila kipimo katika shajara. Ni vizuri kuchunguza afya. Hata kama mtoto wako hana magonjwa ni muhimu kufanya hivyo. Daktari ataweza kumkinga mtoto kwa kumpatia chanjo mbalimbali.
Huduma kwa mtoto
Ni vizuri kupangilia huduma ya mtoto wako mapema. Kuna njia mbalimbali, watoto wenye umri chini ya miaka mitatu (3) wanaweza kwenda kwa waangalizi wa watoto. Wenye umri zaidi ya miaka mitatu wapelekwe shule za watoto au shule za awali (tazama, ”Elimu ya awali”). Watoto wenye umri zaidi ya miaka 6 na 7 wapelekwe shule. Mahudhurio shuleni ni muhimu (tazama,”Mfumo wa Elimu”). Kama ni mfanyakazi unaweza kumpeleka mtoto wako shule za kutwa, au katika vituo vya kuangalia watoto baada ya kutoka shule. Mtoto wako ataweza kukaa hadi saa kumi (10) au saa kumi na moja (11) jioni. Mara nyingi hupata chakula cha mchana hapohapo.
Burudani
Kuna mambo mengi ya kufanya na mtoto wako wakati wa muda wako wa ziada. Kuna viwanja vya michezo vya nje kwa watoto wadogo. Watoto wakubwa wanashauriwa kujiunga na klabu mbalimbali za michezo, kwa mfano; kipindi cha majira ya joto kuna kuna mabwawa ya wazi kila mahali, na mabwawa ya ndani katika majira ya baridi kwa kuogelea. Miji hutoa mikataba maalumu kwa watoto katika likizo ya shule ambayo haina gharama kubwa. Unaweza kupata maelezo kutoka jugendant (katika ofisi za jamii za vijana) na katika kumbi za miji. Klabu nyingi pia zinatoa burudani maalumu kwa watoto (tazama, "Burudani").
Watoto wengi wa Ujerumani wanaadhimisha siku zao za kuzaliwa nyumbani na hufanya sherehe. Wanaalika watoto wengine pia. Ikiwa mtoto wako amepewa mwaliko na kwenda kwenye sherehe Atapata marafiki kwa haraka. Wakati mwingine watoto huwaalika wenzao kwa ajili ya malazi ambayo humwezesha mtoto wako kupata marafiki pia.
Migogoro na unyanyasaji katika familia
Utofauti wa mawazo, wivu au hali zisizotegemewa za maisha zinaweza kupelekea mikwaruzano na migogoro katika familia. Vituo vya ushauri vya wanandoa vinaweza kukusaidia kupata ufumbuzi kwa pamoja. Kwa kuongezea, kuna njia za kujua kuhusu namna ya kupata faraja katika familia.
Wanaohitaji masaada ni wale ambao wamefedheheshwa, kulazimishwa, kutishiwa katika familia zao au ambao wanapata unyanyasaji wa kimwili au kijinsia. Taarifa na namba ya dharura zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya serikali ya mambo ya familia. Pia, kuna ofa za misaada maalumu kwa wanawake.
Video International Sign
Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.
Contact form