Mfumo wa utoaji wa madokezo wa Goethe-Institut
Ukiukaji wowote wa sheria husika unaweza kusababisha madhara - iwe kwa watu wa nje walioathirika, kwa wafanyakazi wa Goethe-Institut au kwa Goethe-Institut kama shirika. Mfumo wa utoaji wa madokezo wa Goethe-Institut hutumika kama mfumo muhimu unaotoa onyo la mapema kwa kugundua mapema ukiukaji wa sheria na kanuni na kuanzishwa kwa hatua zinazofaa za kukabiliana na ukiukaji wa namna hio.
Toa kidokezo
Tungependa kukuhimiza kuripoti dalili zozote za ukiukwaji wa kisheria au udhibiti unaohusiana na kazi ya Goethe-Institut. Mfumo kamili wa mfichuaji unapatikana kwa kusudi hili. Kwa namna ya pekee, mfumo huu unaweza kutumika kutoa taarifa kuhusu:
- Rushwa na utakatishaji fedha
- wizi
- migogoro ya maslahi
- unyanyasaji/ubaguzi
- ukiukwaji wa haki za binadamu
Kila dalili ya utovu wa nidhamu unachukuliwa kwa umakini na kuchunguzwa katika mchakato wenye lengo, uwazi na usio na upendeleo. Utaratibu sanifu umetengenezwa kwa kusudi hili. Kwa habari zaidi, tafadhali rejea
Goethe-Institut itafanya kila kitu katika uwezo wake ili kuhakikisha kwamba mtu anayetoa habari hiyo haathiriwi, mradi habari hiyo imethibitika.
Njia za kuripoti
Mfumo wa kutoa taarifa wa Goethe-Institut una njia zifuatazo za kuripoti:- Tovuti ya kutoa taarifa mtandaoni inapatikana duniani kote, kila wakati na kwa lugha za Kijerumani na Kiingereza. Inaruhusu vidokezo kuwasilishwa bila kujulikana. Ufikiaji wa tovuti ya mtoa taarifa: Goethe Institut e.V. | Startseite (integrityline.app)
- Ripoti za ukiukaji zinaweza kutumwa kwa barua pepe kwa anwani ifuatayo: hinweisgeber@goethe.de au
- kwa barua kupitia anwani ya posta ifuatayo:
Department 70/Risk and Integrity Management
Oskar-von-Miller-Ring 18
80333 Munich
Tafadhali kumbuka kuwa malalamiko kuhusu ubora wa kozi na mitihani yetu hayatashughulikiwa kupitia mfumo wa watoa taarifa wa Goethe-Institut. Ikiwa una malalamiko yoyote kuhusu mitihani au kozi, tafadhali wasiliana na mkuu anayehusika wa idara ya "Kozi na Mitihani" katika taasisi inayoendesha kozi/ mitihani yako.
Maelezo yote kuhusu ulinzi wa data katika utaratibu wa kutoa taarifa yanapatikana hapa.