Kozi ya mtandaoni kwa ajili ya kikundi
Jifunze Kijerumani kwa pamoja - mafunzo ya kusisimua kwa ushirikiano na kwa mtu mmoja mmoja
Wasiliana nasiUmakini na ufanisi
Unapenda kujifunza Kijerumani katika kikundi lakini huwezi kufika katika kituo cha karibu cha Goethe-Institut? Una safari za kikazi na usingependelea kuhudhuria kozi mahali wala kwa muda mahsusi? Endapo ni hivyo, tuna ofa maalumu kwako! Kozi ya kikundi kwa njia ya mtandao ya "Deutsch Online" hukuwezesha kujifunza kwa wakati wako na ratiba yako na haikuhitaji kuwa mahali popote mahsusi. Badala ya kujifunza peke yako, unakuwa sehemu ya kikundi kidogo cha kati ya washiriki 10 hadi 18.
Kusoma, kuandika, kusikiliza, kuongea – Unaamua unavyotaka kujifunza kwa njia ya mtandao. Unachagua kozi ya kikundi au kozi ya mtu mmoja mmoja na kama unapenda kujifunza kwa kujitegemea au kuwa karibu na mwalimu.
-
Ngazi
A1, A2, B1.1, B1.2 -
Inaanza
wakati wowote -
Mda
wiki 10 -
Masaa ya kufundisha ndani ya wiki
mara 2 kwa wiki -
Upeo wa jumla
vipindi 150 vya mafunzo -
Washiriki
idadi ya juu 18 -
Jukwaa la kujifunzia
Kwa kipindi cha kozi -
Bei
TSH 700,000
Jinsi kozi inavyoendeshwa
Jukwaa la mafunzo
Kozi yako ya kikundi ya "Deutsch Online# ipo katika sura tofauti zinazoakisi mada na dhamira za kila siku, na pia itakufundisha matumizi yanayofaa ya msamiati na sarufi. Unajifunza kwa majaribio tofauti kupitia mtandao, kwa mfano video, picha, sauti, kusoma vifungu vya maneno na kujaza nafasi zilizoachwa wazi, kwa kujitegemea mwenyewe na kama kikundi. Tunakupatia maelezo unayoweza kupakua mtandaoni juu ya dhamira tofauti katika kozi ya Kijerumani.
Msaada kutoka kwa mwalimu
Kazi ndefu za kuandikwa zinaweza kutumwa kwa mwalimu kupitia baruapepe, na zitarudishwa zikiwa na masahihisho na mrejesho wa kina. Endapo una maswali yoyote, unaweza kupiga soga na washiriki wengine wa kikundi chako cha “Deutsch Online,” au baruapepe kwa mwalimu wako.
Mafunzo kwa njia ya mtandao kupitia vipindi mubashara
Kutana na mwalimu wako na washiriki wengine katika darasa lako la mtandaoni kupitia mfululizo wa vipindi. Lengo la vipindi hivi ni kushughulikia mahsusi Kijerumani chako cha kuongea.
Huna hakika unatafuta nini? Tuna uhakika tunazo
kozi zinazofaa na zenye kukidhi mahitaji yako.