Taarifa zaidi

Make your mark: the modules

Mtihani wa Goethe-Zertifikat B1 unajumuisha moduli za kusoma, kusikiliza, kuandika na kuongea. Mtihani wa moduli ya kuongea hufanywa katika jozi. Mtihani husimamiwa na kutathminiwa kwa njia ileile duniani kote.
 
Moduli nne zinaweza kusomwa kila moja peke yake au kwa pamoja, na vyeti vinne tofauti kwa kila moduli vikiwa sana na cheti kimoja kwa duru ya moduli zote.
 
Mtihani, ambao ulitungwa kwa pamoja na Goethe-Institut, Chuo Kikuu cha Fribourg cha Switzerland na ÖSD, unajulikana kama Goethe-Zertifikat B1 or ÖSD-Zertifikat B1 na unaweza kufanywa duniani kote.
 

Kusoma

Unasoma maudhui yanayotumwa kwenye blogu, baruapepe, makala ya magazeti, matangazo na maelekezo kwa njia ya maandishi. Unaweza kung'amua taarifa za msingi, maelezo muhimu, pamoja na mitazamo na maoni.

Muda: dakika 65

Kuandika

Unaandika barua/baruapepe za binafsi na za kikazi na kuwasilisha maoni yako kwa maandishi na kutuma mtandaoni.

Muda: dakika 60

Kusikiliza

Unasikiliza matangazo, mihadhara mifupi, mazungumzo yasiyo rasmi na mijadala redioni. Unaweza kunasa ujumbe wa msingi na taarifa muhimu.

Muda: dakika 40

Kuongea

Unaongea na mwenza wako kuhusu mada ya kawaida ya kila siku, mf. Usafiri. Unatoa majibu ya maswali, unaeleza maoni yako na kufanya mapendekezo. Wanafanya wasilisho juu ya mada itokanayo na maisha ya kawaida ya kila siku na kujibu maswali kuhusiana na mada hiyo.

Muda: dakika 15

Mahitaji

Goethe-Zertifikat B1 ni mtihani wa Kijerumani kwa vijana na watu wazima.

Mitihani ya Goethe-Institut hutolewa kwa yeyote anayependa na inaweza kufanywa bila kujali umri au utaifa.
  • Umri wa chini wa miaka 12 unahitajika ili kuweza kufanya mtihani wa Goethe-Zertifikat B1 kwa vijana.
  • Umri wa chini wa miaka 16 unahitajika ili kuweza kufanya mtihani wa Goethe-Zertifikat B1 kwa watu wazima.
  • Ili kufanya mtihani wa Goethe-Zertifikat B1, ni sharti mtahiniwa awe na ujuzi wa lugha ya Kijerumani unaofikia kiwango cha ngazi ya tatu ya umahiri (B1) kulingana na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
  • Ili kufikia ngazi hii, watahiniwa wanapaswa wawe wamekamilisha vipindi  350 and 650 vya dakika 45 za masomo, kwa kutegemea ujuzi wake wao awali na mahitaji yao ya mafunzo.
Juu