Mahali pazuri pa kuanzia: seksheni za mitihani
Mtihani wa
Goethe-Zertifikat A1: Fit in Deutsch 1 unajumuisha seksheni za kusoma, kusikiliza, kuandika na kuongea. Seksheni ya kuongea ya mtihani hufanywa katika kikundi.
Mtihani husimamiwa na kutathminiwa kwa njia ileile duniani kote.
Kusoma
Utatakiwa kusoma maandishi kama vile maelezo mafupi, matangazo kutoka gazetini, utambulisho wa watu, barua rahisi kwenda kwa mhariri au makala fupi kutoka gazetini na kukamilisha majaribio kuhusiana na maandishi haya.
Muda: dakika 20
Kuandika
Utatakiwa kujibu baruapepe, barua, tangazo au aina sawa ya mawasiliano.
Muda: dakika 20
Kusikiliza
Utatakiwa kusikiliza mazungumzo mafupi ya kila siku, ujumbe wa maongezi kwa njia ya simu, taarifa kwa njia ya redio na aina sawa ya taarifa na kukamilisha majaribio kadhaa kuhusina na kile ambacho umesikia.
Muda: dakika 20
Kuongea
Utatakiwa kujitambulisha, kuuliza maswali juu ya mambo ya kila siku na kujibu maswali mepesi. Pia utatakiwa kutoa maombi na kujibizana na mwenzi wako wa mazungumzo kuhusiana na mazingira uliyoyazoea.
Muda: dakika 15
Mahitaji
Cheti cha
Goethe-Zertifikat A1: Fit in Deutsch 1 ni mtihani wa Kijerumani kwa watoto na vijana wenye umri wa miaka 10 hadi 16.
Mitihani kutoka Goethe-Institut hutolewa kwa yeyote anayependa na inaweza kufanywa bila ya kujali kama watahiniwa wamefikisha umri wa chini unaohitajika na pia bila kujali kama wana uraia wa Ujerumani.
- Ili kuweza kupata cheti cha Goethe A1: Fit in Deutsch 1, inashauriwa mtahiniwa awe na umri wa kuanzia miaka 10.
- Goethe-Zertifikat A1: Fit in Deutsch 1 inahitaji ustadi wa lugha kwa kiwango cha ngazi ya kwanza ya umahiri (A1) kulingana na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
- Ili kufikia ngazi hii, watahiniwa wanapaswa wawe wamekamilisha vipindi 80 hadi 200 vya dakika 45 za masomo, kwa kutegemea ujuzi wao wa awali na mahitaji yao ya mafunzo.