Taarifa zaidi

Mahali pazuri pa kuanzia: seksheni za mitihani

Mtihani wa Goethe-Zertifikat A2 unajumuisha seksheni za kusoma, kusikiliza, kuandika na kuongea. Mtihani husimamiwa na kutathminiwa kwa njia ileile duniani kote.

Kusoma

Wanasoma maandishi kama vile makala fupi za magazeti, baruapepe, matangazo ya biashara na matangazo ya kwenye mabango na kufanya uhariri wa maandishi hayo.

Muda: dakika 30

Kuandika

Unaandika ujumbe ambao unahusiana na mazingira yako ya karibu unapoishi.

Muda: dakika 30

Kusikiliza

Unasikiliza mazungumzo ya kawaida ya kila siku, matangazo na mahojiano ya redio, taarifa kwa njia ya simu na matangazo ya hadhara na kufanya uhariri wa taarifa hizo.

Muda: dakika 30

Kuongea

Unauliza maswali na kujibu maswali juu ya mambo yanayokuhusu wewe mwenyewe, unaongelea kitu fulani kuhusu maisha yako na unakubali au kupanga jambo fulani pamoja na mshirika wako wa maongezi.

Muda: dakika 15

Mahitaji

Goethe-Zertifikat A2 ni mtihani wa Kijerumani kwa watu wazima.

Mitihani ya Goethe-Institut hutolewa kwa yeyote anayependa na inaweza kufanywa bila kujali umri au utaifa.
  • Umri wa chini wa miaka 16 unahitajika ili kuweza kufanya Mtihani wa Goethe-Zertifikat A2.
  • Ili kufanya mtihani wa Goethe-Zertifikat A2: Start Deutsch 2, ni sharti mtahiniwa awe na ujuzi wa lugha ya Kijerumani unaofikia kiwango cha  ngazi ya pili ya umahiri (A2) kulingana na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
  • Ili kufikia ngazi hii, watahiniwa wanapaswa wawe wamekamilisha vipindi 200 and 350 vya dakika 45, kwa kutegemea ujuzi wake wao awali na mahitaji yao ya mafunzo.
Juu