Taarifa zaidi

Hatua kwa hatua: seksheni za mtihani

TestDaF ni mtihani uliosanifiwa, uliotungwa na kufanyiwa tathmini centrally ukiwa katika seksheni nne. Ujuzi wako wa lugha utapimwa pembeni kwenye maeneo ya kusoma, kusikiliza, kuandika na kuongea na mara baada ya matokeo yako kukokotolewa, unatunukiwa mojawapo ya ngazi tatu za TestDaF (TDN) za 3, 4 au 5.
 

Kusoma kwa ufahamu

  • Utatakiwa kusoma baadhi ya maelezo mafupi kuhusu maisha ya kila siku ya chuo kikuu, kama vile dondoo kutoka kwenye kama vilemuhtasari wa shughuli za chuo, maelezo mafupi matukio yanayokuja, au kipeperushi, na kueleza maandishi gani yanahusika na jambo lipi.
  • Utatakiwa kusoma maandishi kutoka chombo cha habari (takribani maneno 450–550) yanayoongelea mada ya kisayansi au kijamii na kufanya maswali ya majibu ya kuchagua kuhusiana na maandishi haya.
  • Utatakiwa kushughulikia maandishi yaliyoandikwa kwa kutumia lugha ya kitaaluma (takribani maneno 550–650) kutoka kwa mtaalamu au chapisho la chuo kikuu na kueleza endapo kauli mbalimbali ni kweli au sio kweli au endapo maandishi hayatoi taarifa zozote juu ya kauli hizo.
Muda: dakika 60

Kusikiliza kwa ufahamu

  • Utatakiwa kusikiliza mazungumzo mafupi kuhusu maisha ya kila siku ya chuo kikuu, mf. maongezi baina ya wanafunzi wawili, na kisha kuchukua maelezo juu ya maswali yaliyoulizwa.
  • Utatakiwa kufuatilia mahojiano au mjadala juu ya mada inayohusiana na kozi au mada yoyote  ya kitaaluma na kisha kueleza endapo kauli kuhusu sauti iliyorekodiwa ni kweli au sio kweli.
  • Utatakiwa kusikiliza uwasilishaji au kufanya mahojiano na mtaaluma bingwa na kutoa majibu mafupi kwa maswali yaliyojikita kwenye msingi wa mada.
Muda: takribani dakika 40

Maelezo ya kuandikwa 

  • Utapewa mada na kutakiwa kuandika rasimu ya maandhishi yaliyopangiliwa na kuleta maana kwa msaada wa maswali ya kukuongoza na data za takwimu.
  • Utatakiwa kuchukua msimamo juu ya mada hii na kutetea mtazamo wako.
Muda: dakika 60

Maelezo ya mdomo (mtihani kwa msaada wa kompyuta)

  • Utakabiliana na mambo saba yatakayokuweka katika mazingira tofauti unayoweza kukutana nayo kwenye chuo kikuu nchini Ujerumani.
  • Utatakiwa kupata taarifa, kufafanua maumbo na michoro na kuandika kwa ufupisho maelezo yake. Utatarajiwa kujieleza na kutetea mtazamo wako, kuchukua msimamo, kutoa ushauri, kupambanua chaguzi na kutoa nadharia.
Muda: takribani dakika 35

Mahitaji

Der TestDaF ni mtihani wa lugha unaobainisha kama watahiniwa wana ujuzi wa lugha unaohitajika ili kupata idhini kusoma kwenye chuo kikuu au taasisi ya elimu ya juu nchini Ujerumani. Umekusudiwa zaidi kwa wanafunzi na wengine wenye kupenda kusoma lakini pia unatoa uthibitisho unaotambulika kimataifa kwamba uelewa wako wa Kijerumani unatojitosheleza kufanya miradi ya kisayansi na kujiunga na fani za kitaaluma.
  • TestDaF classifies participants' ujuzi wa lugha kwenye ngazi ya nne/tano ya umahiri (mf. B2 and C1) kama inavyosomeka kwenye Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR). Ili kufanya mtihani, uelewa wako wa Kijerumani unapaswa kufikia walau ngazi ya umahiri ya B2.
  • Kabla ya kujiandikisha kufanya mtihani, watahiniwa wanapaswa kuwa tayari wamekamilisha vipindi 700 hadi 1,000 vya dakika 45 za masomo ya Kijerumani. Siyo lazima kutoa uthibitisho wa uelewa wako wa Kijerumani wakati wa kujiandikisha kufanya mtihani.

Upimaji

Katika seksheni za mtihani wa kusoma kwa ufahamu na kusikiliza kwa ufahamu, alama moja hutolewa kwa kila kipengele kilichokamilika kwa usahihi (mf. maswali yanayofanywa kwa majibu ya kuchagua au kweli/si kweli). Idadi ya vipengele vilivyojibiwa kwa usahihi hutumika kukupanga katika ngazi yako. Seksheni za mtihani wa maelezo ya kuandikwa na maelezo ya mdomo hufanyiwa tathmini na watahini wenye ujuzi na uzoefu na vigezo hutumika kupima kazi yako na kukupanga katika ngazi yako. Maelezo ya kina yanapatikana www.testdaf.de. Unaweza kurudia mtiani kadri upendavyo.

Jiandikishe kufanya mtihani wa TestDaF sasa!

Unaweza kujiandikisha kufanya mtihani wa TestDaF unapokuwa na ufahamu wa kutosha wa Kijerumani. Kabla ya kufanya mtihani wa TestDaF, tunashauri ujizoeshe kwanza na maswali yake. Njia bora ya kufanya hivyo ni kushiriki kozi za maandalizi zinazotolewa na Goethe-Institut vituo vingine. Kozi hizi hukuwezesha kuzoea muundo wa mtihani na namna ya kujibu.

Unaweza kufanya mtihani wa TestDaF sehemu mbalimbali duniani katika siku sita tofauti ambazo hupangwa kila mwaka. Tafadhali tembelea www.testdaf.de to register. Siku maalumu hutumuka kwa Jamhuri ya Watu wa China, ambapo usajili hufanyika kwenye Mamlaka ya Mitihani ya Elimu ya Taifa.

Watahiniwa wenye ulemavu wanapaswa kuviarifu mapema vituo vyao vya mitihani juu ya mahitaji yao maalumu  na kuwasilisha cheti cha hospitali ili mtihani uweze kufanyika kwa njia inayofaa.
Juu