Dhana yetu ya mafunzo
Msingi ni lengo, muundo bayana, mbinu mbalimbali
Mafundisho kutoka Goethe-Institut siyo mafunzo a lugha peke yake, bali pia kufuhamu utamaduni. Tunatumia jaribio la awali la kupima kiwango kwa njia ya kukutana ana kwa ana ili kujua maarifa uliyonayo kabla ya kozi. Tunakusaidia kuchagua kozi inayofaa. Kujua zaidi kuhusu mafundisho ya Kijerumani kutoka Goethe-Institut.
Mafundisho yetu
- huzingatia maarifa ya kisasa katika utoaji wa mafunzo na utafiti wa mafunzo.
- hutumia mbinu mbalimbali na wasilishi. Kuongea, kusikiliza, kusoma na kuandika hufanyika kwa kuzingatia mazingira yatokanayo na uhalisia wa maisha, kwa kutumia maandishi ya kweli.
- huelekezwa kwenye jambo husika la wakati huo na utamaduni. Dhamira zitokanazo na utamaduni mahalia, miradi (mtandaoni) na kazi za utafiti hutoa za aina mbalimbali ya fursa kukabiliana na suala la utamaduni wa watu wanaozungumza Kijerumani.
- Lugha ya kufundishia ni Kijerumani kuanzia somo la kwanza.
- Jukwaa letu la mafunzo hutoa fursa za mafunzo za kibunifu na zenye kunyumbulika.
Mfumo wa kozi zetu
- hutokana na ngazi sita zilizofafanuliwa kwenye Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha. Hii ina maana kuwa ujuzi wa lugha unaopata katika kozi zetu unaweza kupimwa bila upendeleo na kulinganishwa kimataifa.
- umesanifishwa na upo wazi duniani kote. Mara baada ya kumaliza kozi unaweza kuendelea kujifunza kwa namna inayokupendeza – nchini kwako, nchini Ujerumani au kwa njia ya mtandao.
Walimu wetu
- hupewa mafunzo maalumu ya kufundisha Kijerumani kama lugha ya kigeni. Kwa msingi huo, tunatumia programu ya DLL – Deutsch Lehren Lernen (Kufundisha na Kujifunza Kijerumani) ya kukuza weledi, ambayo ilibuniwa na wataalamu wa Goethe-Institut kwa ushirikiano na wawakilishi wa jumuiya ya wanasayansi.
- ongea Kijerumani kama lugha ya asili, au pata ujuzi wa kutosha wa lugha ya Kijerumani.
- pata uzoefu wa kufanya kazi na watu kutoka nchi na tamaduni tofauti.
- hupokea mara kwa mara mafunzo zaidi toka kwetu, hivyo daima huenda sambamba na maendeleo yanayotokea katika kufundisha Kijerumani kama lugha ya kigeni.
- hukupa taarifa za ufanisi wako katika mafunzo kwa utaratibu unaokubalika, na kukushauri jinsi ya kuendelea na mafunzo yako kwa ufanisi.
Mitihani yetu ya Kijerumani
- Mitihani yetu hutambuliwa kimataifa na hukubalika kama uthibitisho wa kuwa na sifa zinazohitajika miongoni mwa waajiri wengi na taasisi za kielimu.
- Mitihani yote ya watu wazima wanaojifunza Goethe-Institut hukaguliwa na Ushirika wa Watoaji wa Majaribio ya Lugha - Ulaya Association of Language Testers in Europe (ALTE) na imetunukiwa ithibati ya ubora kutoka Q-Mark.
Faida za kujifunza nasi
- Uzoefu kamili wa Ujerumani na mambo yake tofauti. Ukijiandikisha kufanya kozi ya Kijerumani kutoka Goethe-Institut, utaweza kutumia maktaba na huduma kwa njia zetu za mawasiliano, pamoja na kuweza kushiriki matukio mbalimbali ya kitamaduni.
- Changamkia huduma zetu za Deutsch für dich bila malipo, zinazokupa uchaguzi wa majaribio na fursa za mawasiliano. Katika jumuiya hii ya watu wanaojifunza Kijerumani una uchaguzi mpana wa kufanya wa nyenzo za mafunzo na majaribio zinazofanya kazi kwa njia ya mwingiliano , na unaweza pia kuongea na wanachama wengine.