Ngazi A1–C2
Kozi za Kijerumani na mitihani

  Matumizi ya awali ya lugha
  A1
Anaweza kuelewa na kutumia misemo ya kila siku na sentensi nyepesi sana zilizozoeleka, zinazohusiana na kutimiza mahitaji yake muhimu. Anaweza kujitambulisha mwenyewe na kuwatambulisha wengine pamoja na kuwauliza mambo yanayowahusu – mf. wanaishi wapi, wanamjua nani na wana nini – na kuweza kujibu maswali ya mtindo huu. Anaweza kuwasiliana kwa njia rahisi endapo watu anaoongea nao wanazungumza taratibu kwa wazi na wapo tayari kumsaidia.
  A2
Anaweza kuelewa sentensi na misemo ya kawaida ya kila siku juu ya mada zinazohusiana moja kwa moja na mazingira yake (mf. taarifa binafsi au taarifa kuhusiana na familia yake, manunuzi, kazi, vitu vilivyomzunguka). Anaweza kujitahidi kueleweka kirahisi, katika mazingira ya kawaida ya kubadilishana kwa njia nyepesi  na moja kwa moja  taarifa juu ya mada za kawaida zinazoongelewa mara kwa mara. Anaweza kufafanua historia na elimu yake, vitu vilivyomzunguka na vitu vingine vinavyohusiana na mahitaji yake muhimu kwa njia rahisi.
  Matumizi huru ya lugha
  B1
Anaweza kuelewa dondoo za msingi pale inapotumika lugha sanifu inayosikika wazi na mtazamo ukiwa kwenye mada zinazoongelewa mara kwa mara kuhusiana na kazi, shule, muda wa kupumzika, nk. Huweza kukabiliana na hali ambazo mara nyingi hukutana nazo wakati wa kusafiri kwenye eneo linalotumia lugha husika. Anaweza kujieleza kirahisi bila kusita juu ya zinazoongelewa mara kwa mara na mambo ambayo binafsi anayapenda. Anaweza kusimulia uzoefu na matukio, kufafanua njozi, matarajio na malengo pamoja na kutoa kauli fupi kutetea au kuelezea mitazamo na mipango yake.
  B2
Anaweza kuelewa maudhui makuu kwenye maandishi changamano juu ya mada na dhana nzito; pia huelewa mijadala ya kitaalamu inayohusiana na eneo lake la msingi la utaalamu. Anaweza kuwasiliana mwenyewe kiasi kwamba maongezi ya kawaida na mwongeaji wa asili kuwezekana kirahisi bila ya upande wowote kutumia jitihada kubwa. Anaweza kujieleza mwenyewe katika uwanda mpana wa mada kwa uwazi na kina, kuelezea mtazamo wake juu ya suala lililotokea na kuonesha faida na hasara za kuchukua uamuzi mbalimbali.
  Matumizi ya kujitegemea ya lugha
  C1
Anaweza kuelewa kwa mapana maandishi marefu yenye changamoto na kung'amua tafsiri zinazojitokeza bila kutajwa. Anaweza kujieleza mwenyewe kwa ufasaha bila ya kutafuta maneno kila mara kwa kuonekana. Anaweza kutumia lugha kwa ufanisi na namna anavyopenda katika maisha ya kijamii na kazi za kitaaluma au kwenye elimu na mafunzo. Anaweza kutoa kauli safi, zilizopangiliwa na zenye maelezo ya kina juu ya mada changamano na kutumia msaada wa maandishi mbalimbali kwa usahihi katika mchakato.
  C2
Anaweza kuelewa bila kupata taabu karibu kila kitu anachosoma au kusikia. Anaweza kufupisha taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya maandishi au sauti, bila kupoteza mantiki au sababu kwenye maelezo. Anaweza kujieleza mwenyewe kwa ufasaha mkubwa na bila kukosea na pia kupambanua kwa uwazi maana tofauti katika mada changamano zaidi.