Taarifa zaidi
Kurudi kwenda Goethe-Zertifikat C1
Hatua kwa Hatua: Moduli
Mtihani wa Goethe-Zertifikat C1 una moduli za kusoma, kusikiliza, kuandika na kuzungumza (mtihani wa watu wawili).
Mtihani huo hutolewa kwa njia ya kidijitali na karatasi katika vituo vilivyochaguliwa vya mitihani. Unafanywa na kutathminiwa ulimwenguni kote kwa viwango sawa.
Kusoma
Unasoma maandishi mbalimbali kama vile makala (za mtandaoni) na makala kutoka kwenye magazeti na majarida. Unapima uwezo wa kurekodi taarifa kuu, taarifa binafsi na maoni.
Muda: Dakika 65
Kuandika
Unaeleza na kutolea sababu maoni yako kwa maandishi katika chapisho la jukwaa kuhusu suala la sasa la kijamii na kuandika ujumbe rasmi. Utatofautiasha toni, mtindo na rejista ili zifae kwa hafla husika na mlengwa husika.
Muda: Dakika 75
Kusikiliza
Utasikia podikasti, mahojiano, majadiliano na hotuba. Unapima uwezo wa kurekodi taarifa, taarifa binafsi na maoni juu ya mada mbalimbali.
Muda: takriban dakika 40
Kuzungumza
Unatoa wasilisho fupi juu ya mada isiyoelezeka kirahisi na kuizungumza na mshirika wako wa mahojiano. Kwa kuongezea, nyinyi wawili mnajadili mada yenye kuleta ubishani.
Muda: Dakika 20
Mahitaji
Mtihani wa Goethe-Zertifikat C1 ni mtihani wa Kijerumani kwa watu wazima.Mitihani ya Goethe-Institut inapatikana kwa mtu yeyote anayevutiwa na unaweza kufanywa bila kujali kama muhusika amefikia umri wa chini kabisa au ana uraia wa Ujerumani.
- Kufanya mtihani wa Goethe-Zertifikat C1, umri wa miaka 16 na zaidi unapendekezwa.
- Kufaulu mtihani wa Goethe-Zertifikat C1kunahitaji ujuzi wa lugha katika kiwango cha umahiri C1 cha Common European Framework of Reference for Languages (CEFR).
- Ili kufikia daraja hili, utahitaji kulingana na ujuzi wako wa awali na mahitaji ya kujifunza - vipindi vya kujifunza 800 hadi 1000, kila kipindi dakika 45.