Taarifa zaidi
Kurudi kwenda Goethe-Zertifikat A1: Start Deutsch 1
Mahali pazuri pa kuanzia: seksheni za mitihani
Mtihani wa Goethe-Zertifikat A1: Start Deutsch 1 unajumuisha seksheni za kusoma, kusikiliza, kuandika na kuongea. Seksheni ya kuongea ya mtihani hufanywa katika kikundi.
Mitihani husimamiwa na kutathminiwa kwa njia ileile duniani kote.
Kusoma
Utatakiwa kusoma maandishi kama vile maelezo mafupi, matangazo kutoka gazetini, vibao vya anuani na mabango na kukamilisha majaribio kuhusiana na maandishi haya.
Muda: dakika 25
Kuandika
Unajaza fomu ya maelezo mepesi na kuandika mwenyewe maandishi mafupi kuhusu hali ya kawaida ya kila siku.
Muda: dakika 20
Kusikiliza
Utatakiwa kusikiliza mazungumzo mafupi ya kila siku, ujumbe kwa njia ya simu au matangazo ya umma kupitia kipaza sauti na kukamilisha majaribio kuhusiana na kile ambacho umesikia.
Muda: dakika 20
Kuongea
Utatakiwa kujitambulisha mbele ya kundi kabla ya kuingia kwenye kipindi cha maswali na majibu kuhusiana na mambo ya kila siku na kuomba chochote kwa mtu mmojawapo kwenye kundi.
Muda: dakika 15
Mahitaji
Goethe-Zertifikat A1: Start Deutsch 1 ni mtihani wa Kijerumani kwa watu wazima.Mitihani ya Goethe-Institut hutolewa kwa yeyote anayependa na inaweza kufanywa bila kujali umri au utaifa.
- Umri wa chini wa miaka 16 unahitajika ili kuweza kufanya Mtihani wa Goethe-Zertifikat A1: Start Deutsch 1.
- Ili kufanya mtihani wa Goethe-Zertifikat A1: Start Deutsch 1, ni sharti mtahiniwa awe na ujuzi wa lugha ya Kijerumani unaofikia kiwango cha ngazi ya kwanza ya umahiri (A1) kulingana na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
- Ili kufikia ngazi hii, watahiniwa wanapaswa wawe wamekamilisha vipindi 80 hadi 200 vya dakika 45 za masomo, kwa kutegemea ujuzi wao wa awali na mahitaji yao ya mafunzo.